JAMAA ANAMSAKA OSAMA BIN LADEN
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgtFtwV9ZLLBsPyOUl0l80QtNs-YuP4BO7GjOgm2JNjUAkrvFjcbwg3wJWYCqoTc7Z6HyAwO7R_P-v0tB9rAcqg2pV67QlcBpZJS0OzQQNXR2kYHqfI20ye6ujgac5-U7HYN2pFMyH-I2aq/s400/4640698.jpg)
Apanga Kumuua Osama Bin Laden kwa Jambia Raia mmoja wa Marekani alijaribu kufanya kile ambacho serikali yake imeshindwa kukifanya kwa miaka kadhaa kwa kuamua kwenda peke yake nchini Afghanistan kumsaka na kumuua Osama bin Laden akiwa na bastola, panga na jambia. Mmarekani Gary Brooks Faulkner mwenye umri wa miaka 52 ametiwa mbaroni nchini Pakistan akiwa kwenye misheni yake ya kumsaka na kumuua kiongozi wa Al-Qaeda, Osama bin Laden. Faulkner alitiwa mbaroni jumapili jioni akiwa kwenye harakati za kuvuka mpaka wa Pakistan kuingia Afghanistan ili kukamilisha nia yake ya kumuua Osama ambaye inasemekana amejificha kwenye milima iliyopo kwenye mpaka wa Afghanistan na Pakistan. Alikamatwa akiwa na bastola moja, panga, jambia na vifaa vya kumwezesha kuona nyakati za usiku. Pia alikuwa na kitabu alichoandika mistari aliyoinukuu toka kwenye biblia. Faulkner ambaye amebatizwa jina la "American Ninja" na magazeti ya Marekani anasumbuliwa na matatizo ya figo na shinikizo la damu, alikuwa ...